Baadhi ya wanafunzi wa kike wakiwa katika moja ya mikutano kuhusiana na udhalilishaji wa kijinsia. Picha ya Maktaba
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kuzuia matukio ya
ujauzito kwa watoto wa kike hali si ya kuridhisha.
Mwaka 2011 idadi ya wanafunzi waliopata ujauzito
ilikuwa ni 13,146, 2012 ikashuka hadi kufikia 11,419, lakini kwa mwaka
2013 idadi hiyo iliongezeka na kufikia 21,420.
Pamoja na kuwepo kwa sababu mbalimbali zinazotajwa
kuwa chanzo cha mimba hizo hususani kwa maeneo ya mijini ni madereva
bodaboda na pamoja na makondakta wa daladala.
Uchache wa maeneo ya ndani ya miji umekuwa ni chanzo cha uanzishwaji wa shule za pembezoni.
Sasa kutokana na mbali wa maeneo zilizopo shule
hizo, watoto hulazimika kutumia vyombo vya usafiri wakati wa kwenda na
kurudi shuleni.
Kwani si jambo rahisi kwa watoto hawa kufika maeneo kama Msongola, Chanika, Mvuti na mengineyo.
Sasa kwa kuwa usafiri unakuwa sehemu ya maisha
yao, madereva na makondakta hao hutumia njia mbalimbali kuwarubuni,
matokeo yake ni kupatikana kwa hizo mimba tunazozungumzia.
Je, makondakta na madereva hao wanaliongeleaje suala hilo?
Juma Mkumba (42) ni dereva wa daladala zinazofanya
safari zake ndani ya Jiji la Dar es Salaam. Anasema hapingani na kauli
iliyotolewa na mkuu wa mkoa kuwa madereva na makondakta ni miongoni mwa
vyanzo vya mimba hizo.
Pamoja na kuwa kitendo hiki hakipendezi hata kidogo kukisikia masikioni, lakini ukweli ni kwamba haya matukio yapo.
“Tumeshuhudia vijana wengi wakianzisha uhusiano na
watoto wa kike. Na pia tumejionea wenyewe wasichana hawa wanavyoishia
kukatiza ndoto za maisha yao kwa kupata ujauzito. Kama mzazi
sifurahishwi kabisa na jambo hili, kwani licha ya kuleta picha mbaya kwa
jamii pia hukwamisha ustawi wa mtoto wa kike na taifa kwa ujumla”
anasisitiza Mkumba.
Wito wangu kwa serikali ni kuwachukulia hatua wale wote wanaowarubuni watoto hawa na hata kuwaharibia maisha yao anasisitiza.
No comments:
Post a Comment