REDUCTION
OF UNPLANNED PREGNANCY ACTION
(RUPA TANZANIA)
RUPA TANZANIA ni shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha
na kupambana dhidi ya mimba na ndoa za utotoni lenye namba za usajili
OOONGO/00007836 chini ya kifungu cha sheria cha mwaka 2002 cha mashirika yasiyo
ya kiserikali limesajiliwa rasmi tarehe 02/03/2015 likiwa na wananyakazi wa
kujitolea tisa(9)
Shirika hili limejiwekea makao yake makuu jijini Dar es salaam wilaya ya
Temeke likiwa na malengo makubwa katika suala zima la kutokomeza kama sio
kupunguza idadi kubwa ya mimba na ndoa za utotoni, kwa kutumia mbinu mbalimbali
ikiwemo ile ya kutoa elimu kila kona ya Tanzania katika ngazi ya shule za
msingi,sekondari na hata majumbani ili kuhakikisha watu wote wanapata elimu
rika na athari zitokanazo na mimba au ndoa za utotoni
WAASISI WA SHIRIKA
Waasisi wa Taasisi hii
ni vijana ambao waliwahi kushiriki program mbalimbali za kuisaidia jamii yetu
ya kitanzania kutoka sehemu mbalimbali katika mikoa ya Tanzania wakiwa chini ya
shirika linaloitwa Raleigh International ambalo
lipo chini ya serikali ya Waingereza pia limefanikisha kuwabadilisha mawazo
ya vijana wengi Tanazania katika suala zima la mipango ya milenia na
kuibadilisha dunia kwa kuwapa elimu mbalimbali katika stadi za maisha na afya
kiujumla ili kuhakikisha dunia ipo katika mikono salama. Miongoni mwa waasisi
hao ni kama wafuatao;
· Emmanuel Agathon Malota-C.E.O
· Patrick Mkama-Assis. C.E.O
· Tito Emmanuel-G.S
· Dorice Ishengoma-Assis. G.S
· Radhia Malla-Assis. Accountant Officer
· Sakina Ishengoma-Program Officer
· Omary Ndete-Member
· Majid Bwangabwa- Member
· Haytoss Ahamad- Member
Hao ndio waliopigana
kikamilifu hadi kuhakikisha Taasisi inasimama kikamilifu ingawa mapungufu kwa
binadamu hayawezi kukosekana na hii inatokana na kuwa hakuna mkamilifu duniani
kote awezae kutenda kila kumpendeza kwa binadamu mwenzake muda na wakati wote.
KAULI DIRA
RUPA TANZANIA pia inaongozwa na kauli
dira yake inayosema’
’mtoto asihukumiwa kuishi katika maisha ya ndoa ama
kupelekea kupata mimba’’
KAULI DHAMIRA
RUPA TANZANIA pia inaongozwa na kauli
dhamira yake inayosema ‘’elimu rika kwa watu wote nchini juu ya athari ya mimba
na ndoa za utotoni’’
RUPA TANZANIA
We believe
We can.
rupa_tanzania@yahoo.com
No comments:
Post a Comment