Meneja wa benki ya NMB tawi la mbagala kitengo cha huduma kwa wateja azungumza na wanafunzi katika swala zima la kujitambua na kufwata yale wanayofundishwa na walimu wao mashuleni, amezungumza hayo jana katika kongamano lililo andaliwa na taasisi moja isiyo ya kiserikali RUPA TANZANIA hapo awali meneja huyo alligusia swala zima la wanafunzi wengi hupoteza muda katika mambo yasiyo na umuhimu ambayo hupelekea wanafunzi wengi kushindwa kufanya vzuri katika masomo yao na mwisho wa siku hujiingiza katika mambo yasiyofaha katika jamii na hupelekea kupata mimba zisizo rasmi kwaupande wa watoto wakike pia meneja huyo aliomba taasisi hiyo isiishie hapo tu kwa upande wa watoto wa kike peke yake wajaribu kuangalia na upande wapili kwani kuna baadhi ya watoto wa kiume wenye umri mdogo wanaonyanyaswa na wakubwa wao na hata wakati mwengine huwa fanyia mambo yaliyo kinyume na maumbile yao alizidi kusisitizia meneja huyo..
Meneja wa Benki ya NMB kitengo cha huduma kwa wateja tawi la mbagala akiongea na wanafgunzi
Pia Dkt Mkuu kitengo cha damu salama katika hospitali ya mbagala chamazi aliwasisitizia wanafunzi hao katika kuwa wavumilivu katika swala zima la maisha kikubwa ni kuzingatia katika masomo kwani wakisoma vizuri na kupata elimu yao ipasavyo basi huko mbeleni wataona matunda yake ya kusoma pia aliwashauri na walimu wao pia kuwapa elimu rika wanafunzi wao wa jinsia zote mbili juu ya athari za ndoa na mimba za utotoni kwani wengi wao siku hizi wanapata mimba na wahusika ni wao kwa wao "unakuta siku hizi kesi nyingi zilizopo mitaani za mimba za wanafunzi wahusika ni wanafunzi kwa wanafunzi ndiyo wanaopeana hizo mimba sasa inabidi walimu na wazazi tuliyopo hapa tushirikiane wote kwa pamoja kuwapa elimu rika vijana wetu hawa"
Dkt mkuu kitengo cha damu salama katika hospitali ya chamazi iliyopo mbagala
No comments:
Post a Comment