Thursday, 19 March 2015

SIKU ZA HATARI ZA KUSHIKA MIMBA NI ZIPI?















 Period


femalereproductiondiagram

Nimeamua kutoa mada hii baada ya kugundua kuwa ongezeko la matukio ya utoaji mimba na kutupa watoto  na hata kuwa na watoto wa mitaani yanasababishwa  zaidi na mimba ambazo hazikutarajiwa.
Mimba nyingine zinaingia kwa sababu mzazi kutokujua siku yake ya hatari ili kujikinga asipate.
Ni muhimu sana kwa mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, mizunguko hiyo iko katika makundi makuu matatu ambayo: Mzunguko mfupi wa siku 25 kurudi nyuma, mzunguko wa kawaida wa siku 28 na mzunguko mrefu wa siku30-35.
Wanawake wengi mzunguko wao  huwa  ni wa kawaida yaani siku 28 hawa ndiyo leo nitawaongelea zaidi.
Ili kutambua mzunguko wako ni wa siku ngapi unatakiwa kuhesabu kuanzia siku ya kwanza kuona damu ya hedhi hadi siku ya kwanza ya kuona damu ya hedhi ya mwezi unaofuata. Kwa mfano ukiona damu ya hedhi tarehe 15 Oktoba  basi hiyo ndiyo siku yako ya kwanza.
Kwa mtu mwenye mzunguko huo wa siku 28 siku zake za hatari za kuweza kushika mimba ni siku ya kumi na nne 14, hivyo kuanzia siku ya 12 hadi siku ya 16 kama atafanya ngono bila kinga anaweza kushika mimba.
Najua mtu anaweza akajiuliza kama siku ya hatari ni ya 14 sasa kwa nini akifanya ngono siku ya 12 anaweza akapata mimba?Hii ni kwa sababu mbegu za kiume zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24 hadi
48 baada ya kujamiiana hivyo kama mwanamke atafanya ngono tarehe 12 na yai likatoka tarehe14 bado litakuta zile mbegu zikiwa hai hivyo zitarutubishwa.

16 comments:

  1. Kwaiyo siku ambozo sio za Hatari ni kuanzia siku ya ngapi adi ngapi

    ReplyDelete
  2. Mbona hujagusia hata kidog kwa wenye mzunguko mrefu jaman

    ReplyDelete
  3. Mimi nimefany ngono taree 12 mwezi wa 12 taree 13 yai likapevuk je hapo mimb itatungwa?

    ReplyDelete
  4. Mm mzunguko wangu unabadilika ni siku 25,26,27 nitawezaje kujua siku yangu ya hatari coz inatokea tu mwezi huu 25 labda mwezi ujao ikarudia 25 mwzi unaofuata zikawa 27 unaofuata 26 yaani hakuna mpangilio maarumu

    ReplyDelete
  5. Me nimeingia period tarehe 19 siku yangu ya hatari ni tarehe ngapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Anza kuesabu kwanza tar 19 sku tano mbele itakua kwny sku zako za hedhi Yan inaisha tar 23 baad ya hapo siku Tano mbele inakua free so kuanzia tar 24-28, alaf sku 10 mbele unakua kwny sku za hatar ukifanya bila Kinga utapata ujauzito ,kwaiy baadae ya kuesabu sku 10, sku ya 10 itadondokea tar 7, baadae ya hapo sku zlzobakia unakua free paka utakapoona mzunguko wako tena, kalibu nikuhudumie sku hzo ambaz uko free

      Delete
    2. Mimi nimeingia period tar 25 nataka kujua siku ya hatar

      Delete
  6. Mimi nimeingia period tar 30 nataka kujua siku ya hatar

    ReplyDelete
  7. Je nimeingia 18_21 mwez wa tatu siku zang za hatar Ni zp

    ReplyDelete
  8. Hy bhn asante mkuu

    ReplyDelete
  9. Siku za hatarii znakuweje hzoo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwakuwa mbegu za kiume zinadumu masaa 24-72 kwa maana ya siku tatu hivyo zinawezakuwepo yai likazikuta kama ilivyo pia zinaweza kuzidi siku 3 baada ya yai kupevuka

      Delete
    2. Je ikiwa mimi ninaingia hedhi siku 15 je naweza kupata mimba siku gani

      Delete
  10. Mimi nmeingia hedhi tarehe 10 nmemaliza tarehe 14 Ni siku zipi?
    naweza nikabeba mimba

    ReplyDelete
  11. Mm nimeingia hedhi tareh 19 natoka tarehe 23 zipi nisiku zahatari kubeba mimba

    ReplyDelete