Tuesday, 10 March 2015

Nchini Tanzania mimba za utotoni hali yasalia tete: UNFPA

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFP leo limezindua ripoti yake na kuitaja Tanzania kama moja ya nchi ambazo zinakabiliwa na ongezeko kubwa la mimba za utotoni na hivyo kuwafanya wasichana wengi kukatiza masomo yao.
Ripoti hiyo ambayo imeangazia hali ya idadi ya watu imesema kuwa kati ya mimba milioni moja zinazotungwa nchini Tanzania, basi asilimia 23 za mimba hizo zinawahusu wasichana walio chini ya umri wa miaka 19. Taarifa zaidi na Chanzo cha Habari
(RIPOTI YA Chanzo cha Habari)
 Kulingana na ripoti hiyo, idadi ya watoto wa kike wanaopata mimba bado ni kumbwa na kwamba takwimu za sasa zinaonyesha kuwa kila kwenye wasichana 10, basi 4 kati yao wamepata mimba.

Baadhi ya mambo yaliyotajwa kusababisha hali hiyo ni pamoja na kuwepo kwa mila potofu ambazo zinawakandamiza na kuwabagua watoto wa kike.

Jambo jingine lililoelezwa na ripoti hiyo ni kuendelea kuongezeka kwa ndoa za utotoni ambazo hutumika kama kigezo cha kujipatia mali kwa baadhi ya wazazi.
Akielezea zaidi kuhusiana na hali hiyo, Afisa wa UNFPA anayeshughulika na afya ya uzazi Dorothy Temu Usiri kutokana na ukubwa wa tatizo hilo, tayari kumeanzisha kampeni zinazotaka kuangaliwa kwa sheria ya ndoa ambayo itaruhusu mtoto wa miaka 15 kuolewa.

No comments:

Post a Comment