Sunday, 29 May 2016

Taasisi isiyo ya kiserikali RUPA TANZANIA yajumuika na wanafunzi katika kukamilsha agizo la mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda katika kufanya usafi..

Kama ilivyo kawaida katika mkoa wa Dar es salaam kila ifikapo mwisho wa mwezi huwa ni siku ya usafi kimkoa mzima wa Dar es salaam ilikukamilisha agizo la mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda katika siku hiyo taasisi moja isiyo ya kiserikali  RUPA TANZANIA ilikamilisha agizo hilo kwa kujumuika na wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari  katika kufanya usafi maeneo tofauti tofauti ya wilaya ya temeke..Hapo chini ni baadhi ya matukio katika picha.
 

 
Baadhi ya wanafunzi toka shule mbali mbali za msingi na sekondari waliojumuika pamoja na wafanyakazi wa RUPA katika swala zima la usafi katika kukamilisha agizo la mkuu wa mkoa Mh. Paul Makonda, usafi huo ulifanyika katika maeneo ya chang'ombe wilaya ya temeke mkoa wa
Dar es salaam...



 Baadhi ya wanafunzi wakionekana wenye furaha huku wakielekea katika maeneo mbali mbali waliopangiwa na viongozi wao katika shughuli nzima ya usafi...


Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari chang'ombe na chamazi wakiwa katika maeneo ya ofisi ya serikali za mitaa za keko wakifanya usafi...
  


 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi matitu na kilamba wakiendelea na zoezi zima la usafi..

 


  Baadhi ya viongozi na wanafunzi wakitoka katika maeneo waliofanya usafi..

No comments:

Post a Comment