Katika swala zima la kumsaidia kumjenga mtoto wakike katika kushinda vishawishi na mambo mabaya yanayo wakabili hasa swala zima la ndoa na mimba za utotoni ambapo jamii nyingi ya kitanzania limekuwa sugu kuanzia mijini hadi vijijini. Kutokana na swala hilo taasisi ya RUPA TANZANIA ikishirtikiana na asasi nyingne zisizo za kiserikali na kiserikali pia jana lilifanya kongamano liitwalo SAUTI YA MTOTO WA KIKE la kupinga vikali vita hivyo ambapo lilipata kuudhuriwa na baadhi ya wanaharakati wanaosaidia kupigana na matatizo hayo katika jamii inayotuzunguka..Kwani mtoto wakike ndiyo chanzo cha kujenga familia katika jamii...
Baadhi ya matukio ya kongamano la SAUTI YA MTOTO WA KIKE katika picha lililofanyika hapo jana katika ukumbi wa duce changómbe wilayani temeke mkoa wa Dar es salaam...
Baadhi ya wafanyakazi wa shirika la RUPA TANZANIA, Kutoka kulia ni Bi Rehema, Bi Waldah Faham, Bi. Fatmah Mukharamy, Ndg Lazaro Musalaka, Bi. Christina Nguyu. Hao ni baadhi ya watumishi wa Rupa Tanzania.
No comments:
Post a Comment